Alhamisi 16 Oktoba 2025 - 23:40
Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa kiongozi mahiri na shule hai ya muqawama

Hawza/ Sayyid Abulhasan Miri, afisa wa kitamaduni na mkuu wa nyumba ya utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Quetta, Pakistan, amemuelezea Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah kama kiongozi wa kihistoria na mfano hai wa mapambano dhidi ya dhulma, uvamizi na ubeberu wa kimataifa, akisisitiza juu ya kuendelezwa kwa njia na falsafa ya muqawama.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kauli hiyo ilitolewa katika kongamano maalum lililoandaliwa kwa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi “Kiongozi wa Muqawama” Sayyid Hassan Nasrallah (r.a) pamoja na wafuasi wake, lililofanyika kwa juhudi za nyumba ya utamaduni ya Iran mjini Quetta.

Sayyid Abulhasan Miri alieleza kuwa shahidi huyo alikuwa kiongozi wa kipekee wa mstari wa mbele wa muqawama, ambaye kwa zaidi ya miongo mitatu alitumia hekima, ujasiri na uongozi wa kimkakati kupambana na mfumo dhalimu wa ubeberu wa kimataifa.

“Kwa utashi na azma yake thabiti, aliutikisa mfumo wa kidhalimu wa dunia na hatimaye akapata ndoto yake ya muda mrefu — medali ya milele ya shahada. Uislamu ulimwengu mzima uliingia katika huzuni kubwa,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa zaidi ya kiongozi wa kisiasa au kijeshi; alikuwa mbunifu wa mabadiliko makubwa katika mizani ya nguvu za eneo la Asia Magharibi. Uwepo wake ulikuwa ni hatua muhimu katika historia ya kisasa ya ulimwengu wa Kiislamu.”

Akirejea ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, Sayyid Ali Khamenei, ulioelezea sifa nne za Nasrallah, alisema: “Kiongozi huyo mkuu alimuelezea Sayyid Hassan Nasrallah kuwa ni mujaahid mkubwa, mbeba bendera wa muqawama katika eneo, mwanazuoni mwenye elimu ya dini na kiongozi mwenye busara za kisiasa. Alisema pia kwamba ‘Sayyid wa Muqawama’ hakuwa mtu tu, bali alikuwa njia na shule, na shule hii itaendelea kuishi.”

Sayyid Miri alifafanua kuwa mafundisho ya shule ya Sayyid Hassan Nasrallah yanajikita katika vipengele vitatu muhimu:

1. Ujasiri na uthabiti: Nasrallah alikuwa mfano halisi wa ushujaa wa Ahlulbayt (a.s), hususan Imam Hussein (a.s). Hakuwahi kuogopa vita wala kifo, na alijitolea nafsi yake yote kwa ajili ya uhuru wa Palestina na ulinzi wa heshima ya Lebanon.

2. Busara na hekima: Alikuwa kiongozi mwenye akili timamu, ambae hakuruhusu hisia au msisimko wa kisiasa kuathiri maamuzi yake. Na kila alipokosea katika mbinu au mikakati, alikiri kwa unyenyekevu.

3. Uhusiano wa karibu na kituo cha muqawama – Iran na Kiongozi Walii al-Faqih: Alikuwa kiungo muhimu katika umoja wa muqawama wa Kiislamu.

Mwisho, Miri alisema kuwa leo muqawama umepevuka na umejitegemea kwa “nadharia na programu zake za kimfumo.” Kwa hivyo, kuwepo au kutokuwepo kwa viongozi wakubwa kama Shahidi Qasem Soleimani, Sayyid Hassan Nasrallah, Ismail Haniyeh, au Yahya al-Sinwar, hakutavunja wala kudhoofisha mwendelezo wa harakati ya muqawama.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha